Je umepoteza dira
Mbele huoni unaona giza
Utawezaje unajiuliza
Lakini nataka mimi kukujuza
Kwamba Yesu wa miujiza
Anasema uje kwake
Siku mpya imekuja
Nuru yako imezuka
Asubuhi imefika
Inuka wewe shujaa
Umelialia vya kutosha
Inuka
Usiogope, (Wewe wewe)
Usikate tamaa, (Wewe wewe)
Usiogope, (Wewe wewe)
Usikate tamaa, (Wewe wewe)
Kuna muda unajiona hufai
Lakini kumbe Mungu anakusudi
Vile uonavyo leo
Siyo tamati ya kesho
Tumaini bado lipo
Usiogope, (Wewe wewe)
Usikate tamaa
Usiogope, (Wewe wewe)
Usikate tamaa, (Wewe wewe)