Haya maisha huweza kukupitisha
Mahali pagumu sana mpaka
Utamani kutelekeza vitu
Na upotee kabisa
Moyo umenyong'onyea kila kitu
Hakiendi ulivyopanga
Na wakati huu Mungu anakutazama
Hatua utakayoichukua
Usiumize kichwa Usiumize kichwa
Rudi kwake Yesu Anayo majibu
Ya maswali yako atakupa amani
Ya Moyo wako na kufungua milango
Sikia sauti ya roho mtakatifu
Inaposema nawe Akili
Hupotoshwa na Shetani
Hupoteza mwelekeo mkabidhi
Mungu maisha yako yote
Na ushukuru kwa vyote
Anapokupitisha kunayo sababu
Ya kila hatua ya maisha yako
Usiumize kichwa Usiumize kichwa
Rudi kwake Yesu Anayo majibu
Ya maswali yako atakupa amani
Ya Moyo wako na kufungua milango