Upendo wako wanijaza na furaha
Neno lako ndilo nguzo na silaha
Yesu wewe watosha
Yesu Mchungaji wangu
Sitapungukiwa na kitu
Kando ya maji matulivu huniongoza
Pokea dhabihu yangu
Na wimbo wa moyo wangu
Maisha nakutolea
Niongoze unavyo penda Eh Bwana
Wewe ndiwe tumaini la uzima
Ahadi zote ni za milele
Yesu Wewe watosha
Yesu Mchungaji wangu
Waburudisha nafsi yangu
Kikombe changu kimejazwa vizuli
Pokea dhabihu yangu
Na wimbo wa moyo wangu
Maisha nakutolea
Niongoze unavyo penda Eh Bwana
Nitaimba sifa zako bwana
Nitaimba tenzi za rohoni
Umetenda mambo makuu
Wewe ndiwe njia na uzima
Pokea dhabihu yangu